BADO SIKU 06 TU KUFANYIKA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI
"Utoaji wa takwimu sahihi utarahisisha Serikali kupanga mipango yake endelevu kwa wananchi wake kama kuwajengea barabara, zahanati, shule na maji kulingana na idadi yao na kiwango cha uchumi wao"
Hayo ni maneno ya Isaka Mwambepo mkazi wa Kyimbila kata ya Msasani Wilayani Rungwe.
Zoezi la sensa ya watu na makazi linatarajia kufanyika siku ya jumanne tarehe 23.8.2022 na litahusisha utoaji wa taarifa sahihi dhidi ya mtu aliyelala katika kaya husika au kaya za jumuiya kama gereza, hospitali, vituo vya watoto yatima, mabweni ya wanafunzi, stendi za garimoshi, mabasi, viwanja vya ndege, bandari, Kambi za wavuvi na wapasua mbao.
Taarifa zitatolewa kwa karani wa sensa kwa kutumia utaratibu ulioandaliwa na kamati ya sensa ngazi ya Wilaya, Kijiji, mtaa/kitongoji na shehia kwa upande wa Tanzania visiwani.
Mkuu wa kaya atatakiwa kuhakikisha anakuwa na taarifa muhimu za watu wote kama umri, elimu, jinsi, hali ya ndoa, umiliki wa kitambulisho cha taifa na shughuli za kiuchumi.
Siku ya tarehe 23/8/2022 karani wa sensa ataongozana na Mwenyekiti au kiongozi wa Serikali ya mtaa/ kitongoji katika kaya akiwa na kitambulisho Cha karani wa Sensa na Dodoso la Sensa lililowekwa katika kifaa Cha kielektroniki kiitwacho Kishikwambi ( Tablet) na kuuliza maswali yatakayojibiwa na Mkuu wa kaya.
Iwapo mkuu wa kaya hatakuwepo mtu mingine yeyote mzima katika kaya na mwenye taarifa sahihi kuhusiana na kaya husika dhidi ya watu waliolala katika kaya husika atasaidia kujibu maswali kwa niaba ya Mkuu wa kaya.
Ikumbukwe kuwa taarifa zitakazotolewa na Mkuu wa kaya kuwa ni SIRI na zitatumika kwa madhumuni ya takwimu/ Sensa tu.
Usikose kusikiliza kipindi cha Sensa kwa Maendeleo kesho tarehe 17 .8.2022 kupitia Rungwe FM 102.5 MHz saa 12:00 jioni.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa