Siku chache zilizopita afisa maendeleo ya jamii (W) ya Rungwe bwana Omary Mungi alizitambulisha asasi zisizo za kiserikali ambazo zitawajengea uwezo vijana katika stadi za afya ya jamii, uongozi bora na ujasiriamali.
Mapema leo asasi ya Youth education through sports (YES Tanzania) imekutana na watendaji wa kata za Nkunga, Lupepo, Swaya,Ikuti, Bujela, Suma na Masebe ambako huko watajikita na mafunzo ya uongozi bora kwa vijana huku wakitoa kipaumbele kwa vijana wa kike.
.Akitoa maelezo zaidi Mkurugenzi Mtendaji wa YES Tanzania bwana Kenneth Simbaya amesema kuwa kijana akijitambua atafanya jambo sahihi kwa wakati sahihi na hivyo kuleta ufanisi kwa jamii husika.
Aidha amesema kuwa lengo la YES Tanzania ni kuwajengea uwezo vijana kushirikiana na viongozi wa vijiji ili kuleta tija na jamii endelevu katika nyanja ya afya, uongozi na ujasiriamali.
Pamoja na hayo bwana Simbaya amesema iwapo mtoto wa kike atapewa mafunzo stahiki atailetea jamii manufaa lukuki ikiwa ni pamoja na kuondoa utapiamulo kwa familia, kushiriki uzazi wa mpango, ujasiriamali na kuondokana na tamaduni kandamizi kwa wanawake
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa