MIAKA MIWILI YA MAMA: TUNATELEZA MPAKA BUSOKELO
Katika awamu hii ya sita Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Tukuyu mjini hadi Busokelo.
Kwa sasa ujenzi upo hatua ya ukamilishaji kwa umbali wa km 07 kuanzia Tukuyu hadi Ntandabala-Pakati kata ya Masoko. Kwa upande wa Busokelo barabara ipo hatua pia ya ukamilishaji kuanzia Lwangwa hadi mto Mbaka (Mbambo).
Barabara hiii itakapokamilika itaondoa changamoto ya usafiri na kutembea umbali mrefu kufuata huduma mbalimbali kama elimu, afya, bidhaa za viwandani, kilimo, na utawala.
Mathalani nauli kutoka Halmashauri ya Busokelo(Lwangwa) mpaka Tukuyu mjini kwa abiria mmoja ni shilingi 5000. Barabara hiii itakapokamilika gharama itashuka zaidi ambapo salio litakalobaki mkazi atalitumia kwa ajili ya huduma zingine kama afya, kulipia ankara za umeme, maji, ada ya wanafunzi, kununua chakula, na mengine mengi.
---ASANTE MAMA-
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa