Kata ya Kiwira imekabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi Million 10 ikiwa ni ahadi aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo mapema siku ya jumapili tarehe 07.8.2022.
Katika ziara hiyo Mhe. Rais aliahidi kuichangia kata hiyo kiasi cha shilingi Million 10 ikiwa ni juhudi ya kuunga mkono nguvu za wananchi huku akiagiza wizara ya TAMISEMI kuhakikisha inakipelekea kituo hicho fedha za ziada ili kukamilisha ujenzi mapema.
Akikabidhi hundi hiyo, Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe.Dkt Vicent Anney amemshukuru Mhe. Rais kwa hekima aliyoionesha kwa wakazi wa kata hiyo kuwa kwa kufanya hivyo changamoto ya matibabu itaenda kumalizika kwa kufuata huduma ya afya umbali mrefu hususani kwa Mama na watoto.
Aidha ameagiza kamati ya ujenzi, na mapokezi kufanya kazi kwa weledi ili kazi hiyo imalizike kwa wakati na hivyo kutoa fursa ya kituo kuanza kutoa huduma mapema zaidi.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga ameahidi kuwa Halmashauri itatoa kiasi cha Shilingi Million 10 ikiwa juhudi za Kummunga mkono Mhe.Rais kwa moyo wa upendo kwa wakati wa kata ya kiwira aliouonesha.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ameahidi kusimamia ipasavyo ujenzi wa kituo hicho na kumalizika kwa wakati ikiwa ni juhudi ya kuhakikisha wakazi wote wilayani Rungwe wanapata huduma ya matibabu stahiki katika maeneo yao na hivyo kupata afya bora itakayowawesha kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
Naye Diwani wa kata hiyo Mhe. Michael Mwamwimbe amemshukuru Mhe. Rais kwa msaada huo alioutoa na kuwa ataendelea kuwaunganisha wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama vyao na hivyo kupanua wigo wa maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe Bwana Sam Mwakapala ameongoza Harambe kwa ajili ya Ujenzi wa kituo hicho ambapo jumla ya shilingi laki 2.1 zimekusanywa huku akisisitiza wakazi wa kata hiyo kushikamana na kuachana na siasa za kubaguana kwa itikadi ya vyama hali itakayochochea kurudi nyuma kimaendeleo.
"Daima CCM inatekeleza ilani yake kwa vitendo na matunda ndiyo haya mnayaona na niwaahidi UVCCM itakuwa bega kwa bega kuhakikisha kituo hiki kinakamilika kwa wakati" amesisitiza.
Halmashauri ya Rungwe imejenga vituo vingi kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa watu wake. Vituo hivi ni pamoja na Ikuti, Mpuguso, Isongole, Kalebela na Masukulu. Vituo ambavyo vipo katika hatua ya ukamilishaji ni pamoja na Iponjola, Kyimo, Ndanto, na Swaya.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa