• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Rungwe District Council
Rungwe District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, U mwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafishaji na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Tehama na Mahusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Utunzaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Uzalishaji wa Maziwa
    • Kiwanda Cha Matunda
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Ardhi na Maliasili
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
      • Mikutano ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Katiba Pendekezwa
    • Mihutasari
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Matukio
    • Habari
    • Makala

ALIYECHOMA PICHA YA RAIS JELA MIAKA MIWILI

Imewekwa Tarehe: July 4th, 2024

Mahakama ya wilaya ya Rungwe mapema leo julai 4. 2024 imemtia hatiani Bw. Shedrack Yusuph Chaula mwenye umri wa miaka 24 kutumikia kifungo cha miaka miwili (2) gerezani au kulipa faini ya shilingi millioni 5 kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandaoni 2015.


Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali Rosemary Mgeniji mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Mh. Ramla Shehagiro ameeleza kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo 22/6/2024 katika kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka kuwa mshtakiwa huyo akiwa dukani kwake maeneo ya Ntokela alirekodi ujumbe wa video wenye maneno“Kwakua umeshindwa kutetea taifa lako lisiathirike na ushoga hii video inakuhusu wewe na si mtu mwingine”  huku akijua kuwa  taarifa  hizo ni za uongo zenye kupotosha jamii.


Alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo mtuhumiwa huyo Bw. Shadrack Chaula mkazi wa Ntokela amesema yupo tayari kutumikia adhabu yoyote atakayopewa na mahakama hiyo.


Upande wa jamhuri ukiongozwa na mawakili wa serikali Veronica Mtafya na Rosemary Mgeniji umeiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kwani kitendo hicho kimetafsiriwa kama udhalilishaji kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akitoa hukumu hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Ramla Shehagiro amesema kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 16 amemtia hatiani kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni tano.


Hata hivyo mtuhumiwa amepelekwa gerezani kwenda kutumikia kifungo baada ya kushindwa kulipa faini.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE SEMINA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR December 19, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA AKIBA NAFASI YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI December 19, 2024
  • TANGAZO BARAZA LA MADIWANI April 27, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MKATABA June 10, 2021
  • Onesha Vyote

Habari Mpya

  • BLAC MAENDELEO YAHITIMISHA MAFUNZO KWA WAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE

    May 02, 2025
  • CHANJO YA POLIO KUTOLEWA MEI MOSI

    April 16, 2025
  • KAMATI YA SIASA YAPONGEZA MIRADI

    April 15, 2025
  • MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YAWANUFAISHA WANANCHI

    April 07, 2025
  • Onesha Vyote

Video

Vivutio vya Utalii
Picha Mjongeo Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • TAMISEMI

Vinganishi Linganifu

  • OR TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Ufundi
  • Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma

Kipimo cha Wateja Duniani

world map hits counter

Wateja Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB

    Sanduku la Posta: Box 148

    Simu: 025 255 2586

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Huruhusiwi
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa