Ugonjwa huu uligundulika nchini Kenya mwaka 1910. Kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ugonjwa huu uliingia kupitia Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya ukitokea Mkoa wa Kalonga nchini MALAWI.
Dalili zake ni nguruwe kupata homa kali, Ukurutu, Damu kuvia katika Ngozi, Kukosa hamu ya kula, kinyesi chenye damu, kutupa mimba na kutapika.
Ugonjwa huu hauna tiba wa kinga
NAMNA YA KUUDHIBITI
1. Jenga banda la kufugia nguruwe kulingana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo. usitumie ufugaji huria.
2 Tengeneza sehemu ya kuwekea dawa ya kukanyaga wakati unaingia na kutoka kwenye banda
3. Watu tofauti na mhudumu wasikaribie au kuingia katika banda la nguruwe
4.Nunua nyama au nguruwesehemu zinazofahamika kutokuwa na homa ya nguruwe na zingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo
5. Usichanganye nguruwe wageni na wenyeji.
6. Usiuze wala kuhamisha nguruwe wagonjwa au waliogusana na wagonjwa.
7.Chakula cha nguruwe lazima kitoke katika maeneo ambayo hayana magonjwa.
8. Toa taarifa za vifo kwa mtaalamu wa mifugo
9. Nguruwe waliokufa kwa ugonjwa wa homa ya Nguruwe wafukiwe kwenye shimo refu
10. pulizia dawa mara kwa mara kulingana na ushauri wa mtaalamu
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa