1.Hakikisha kazi yako inakuwa safi/ nadhifu ili kumvutia msahihishaji.
2. Amini kuwa majibu yako ni sahihi zaidi, usidhani ya jirani yako ni sahihi kuzidi yawezekana ndo amekosea zaidi kukuzidi wewe. Jiamini kuwa wewe unaakili kuzidi jirani yako.
3. Hakikisha michoro yote unachora vizuri kwa usafi kwani ina nafasi kubwa kukuongezea alama na ushindi.
4.Hakikisha unamaliza maswali yote kadri ulivyoelekezwa kwani kushindwa kufanya hivyo ni ngumu kupata alama za juu za ushindi.
5.Ukiingia kwenye chumba cha mtihani usianze kufanya mtihani, tulia, vuta pumzi, jinyoshe, sikiliza maelekezo ya msimamizi wa mtihani, kisha pitia maswali yote kwa usahihi na rudiarudia tena kupata dhana (concept) halisi na mbinu zilizofumbwa.
6.Chukua kalamu yako na tiki maswali yote unayojua.
7 Anza na maswali unayoyajua kisha malizia na maswali magumu.
8. Ikiwezekana fanya maswali yenye maksi nyingi zaidi kabla ubongo haujachoka na unakumbuka vitu vingi na kisha malizia yenye maksi hafifu.
9.Usiingie na makaratasi (cheating aid) yenye sura ya udanganyifu kwani unaweza kufutiwa matokea na kuharibu maisha yako.
10. Kwa somo la HESABU unapoanza mtihani, andika kanuni/ fomular muhimu zote nyuma ya karatasi kwa hiyo itakuongezea kujibu maswali kiurahisi.
11.Usijali kama wengine wanamaliza kabla yako, yawezekana wameshindwa sasa wewe una nafasi ya kupata ushindi.
12. Usiigilizie/ Kunakili kwa jirani yako majibu yawezekana mwanafunzi kando yako amejibu visivyo.
13. Ukiwa na muda, angalia mtihani/ majibu yako tena. Tafuta makosa uzembe.
14. Usipolijua jibu liruke halafu rudi baadaye. mara nyingine unaweza kutafuta jibu katika vipande vingine vya mtihani.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa