YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kupata kibali cha ajira Mbadala Kumb.Na.FA.170/364/01/131 cha tarehe 05 Agosti, 2019 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhusu ajira mpya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili:-
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
Hati za Matokeo za kidato cha nne na cha sita (Form IV and Form VI RESULTS SLIPS) HAZITAKUBALIWA. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA).
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika Utumishi wa umma waombe kwa kuzingatia maelekezo yaliyomo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010 (Wapitishe maombi yao kwa Waajiriwa wa sasa).
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni 30/09/2019
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kii ngereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE
S.L.P. 148
TUKUYU/RUNGWE
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY III) NAFASI MOJA (1).
MAJUKUMU YA KAZI
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
Kupokea wageni, kuwasahili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anamofanyia kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada/nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo Ofisini.
Kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu Taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
Kusaidia kupokea majalada kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
MSHAHARA
AFISA MTENDAJI WA KIJIJI III(VILLAGE EXECUTIVE OFFICER III) – NAFASI MOJA (1)
MAJUKUMU YA KAZI
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita(VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Imetolewa na
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa