Uongozi na Utawala Idara ya Elimu Msingi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Msimamizi mkuu wa Idara na Vitengo vyake katika kazi za kila siku.
Mdhibiti wa matumizi ya fedha za Idara kwa kuzingatia kanuni za matumizi ya fedha za Serikali.
Msimamizi mkuu wa mikakati na mbinu za kuinua kiwango cha Taaluma katika Wilaya.
Msimamizi mkuu wa shughuli za uboreshaji majengo, miundombinu na mazingira ya shule Wilayani.
Msimamizi mkuu wa upatikanaji wa haki, maslahi na ustawi wa walimu Wilayani.
Kusimamia maadili, nidhamu na uwajibikaji wa walimu shuleni na walimu ofisini (Maafisa Elimu na Waratibu Elimu Kata).
Kusimamia uhamisho na uhamishaji wa walimu ndani na nje ya Wilaya.
Kusimamia idhini ya kwenda mafunzoni walimu na ofisini.
Kusimamia mapendekezo ya Waratibu Elimu Kata, TRC na walimu wakuu na kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Kusimamia OPRAS kwa Idara ya Elimu Msingi.
TAALUMA
Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi;
Kushiriki katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza;
Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini mitihani ya Darasa la Nne na Saba, pamoja na mitihani ya Ualimu na Ufundi katika Wilaya akishirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM – TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi(WEMU);
Kubuni mipango ya kuinua kiwango cha taaluma katika Halmashauri na kusimamia utekelezaji wake;
Kukusanya, kuchanganua, kutuma na kutoa takwimu sahihi;
Kubuni mipango ya kuimarisha na kuendeleza taaluma ya walimu na wanafunzi;
Kuratibu mashindano ya taaluma yanayoendeshwa katikaWilaya;
Kuratibu utoaji wa huduma muhimu kwa wanafunzi kama vile mahudhurio, uhamisho na huduma za chakula;
VIFAA NA TAKWIMU
Kukusanya na kuratibu takwimu za kielimu.
Kupokea, kuchambua na kuratibu taarifa za mwezi,robo mwaka,nusu mwaka na mwaka.
Kupokea na kusimamia fedha za ruzuku ya uendeshaji shule[capitation grants] na maendeleo[development grants]
Kusimamia na kuratibu ujenzi wa miundombinu ya shule.
Kupokea na kuratibu taarifa za PEDP.
Kuratibu usajili wa wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza.
Kuratibu na kusimamia vifaa vya Elimu.
Kuratibu mtihani wa Taifa wa darasa la IV na VII.
Kuratibu utoaji wa chakula shuleni.
ELIMU MAALUM
Kukusanya ,kuchanganua na kutuma takwimu sahihi za wanafunzi wenye ulemavu kuanzia shule za msingi sekondari na watu wazima.
Kubuni mipango ya kuimarisha na kuendeleza upatikanaji wa mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kuratibu na kusimamia mafunzo kazini ya walimu wataalam wa elimu maalum.
Kusimamia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni.
Kusimamia uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kuanzia shule za msingi hadi sekondari.
Kufanya upimaji wa kina ili kubainisha viwango vya ulemavu kwa wanafunzi na kutoa huduma kulingana na mahitaji yao.
Kufanya kazi nyingine zitakazoagizwa na mkurugenzi na wakuu wa idara ya msingi na sekondari.