SOKO LA NDIZI LA KISASA KUJENGWA KIWIRA
Noah Kibona, RUNGWEDC
Zabuni ya ujenzi wa soko la ndizi la kisasa tayari imetangazwa kupitia mifumo ya Manunuzi (NesT) pia inapatikana katika tovuti ya www.rungwedc.go.tz
Soko hili linajengwa eneo la Karasha kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira
Ujenzi wa soko hili pamoja na mambo mengine itaongeza thamani ya zao hili la chakula na biashara kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe
Aidha litaboresha bei ya ndizi pamoja na ukusanyaji wa mapato ya serikali
Kwa mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imezalisha kiasi cha tani 729,092.80 za ndizi hatua iliyofungua masoko nje na ndani ya nchi
Soko hili sasa kitakuwa kitovu cha upatikanaji wa ndizi na hivyo kuepusha wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakiwanyonya wakulima.
Pamoja na hayo soko litakuwa na Maduka ya kisasa, hoteli, Maegesho, Vyumba baridi (Coldroom) kwa ajili ya kuhidadhia ndizi.
Mpango wa serikali ni kujenga Masoko mengine kama haya wilayani Rungwe katika awamu pili lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa