• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Rungwe District Council
Rungwe District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, U mwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafishaji na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Tehama na Mahusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Utunzaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Uzalishaji wa Maziwa
    • Kiwanda Cha Matunda
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Ardhi na Maliasili
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
      • Mikutano ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Katiba Pendekezwa
    • Mihutasari
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Matukio
    • Habari
    • Makala

LISHE BORA KWA MAISHA YETU

Imewekwa Tarehe: May 5th, 2020

LISHE BORA KWA   MAISHA YETU

Noah kibona, Rungwe Dc

Imeelezwa kuwa uzingatiaji sahihi wa lishe katika ngazi ya kaya huchochea  ustawi bora wa jamii ukiwemo ukuaji wa ubongo na afya ya mwili.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Rungwe Bibi Loema Peter wakati akiongea na wadau wa Lishe Ofisini Kwake ambapo  pamoja na mambo mengine amesisitiza  jamii kuzingatia chakula chenye viini lishe.

“Inashangaza kuona watoto wanapata Udumavu na Utapiamlo ili hali wilaya ya Rungwe inazalisha  vyakula vya aina mbalimbali” aliongeza Bi. Loema. Kutotilia mkazo katika kilimo, ufugaji  mazoea wa wanyama  na  mazao ya nyuki kumechangia baadhi ya familia kukumbwa na magongwa nyemelezi yatokanayo na  ukosefu wa lishe.

Wilaya ya Rungwe inayopatikana  katika latitude 9 o 00 ′ na  9 o 30 ′ E na longitude  33 o , 34 o S na eneo la mraba, kilometa zipatazo  2 221 lenye mwinuko wa 770 m a.s.l to 2 265 m a.s.l,  inaiwezesha wilaya hii kupata mvua nyingi zinazochochea kulima mazao ya mizizi kama karanga, viazi vitamu na mviringo, magimbi na njugu. Matunda kama ndizi, mananasi na maparachichi hupatikana kwa wingi pia. Mahindi, mpunga na mihogo pia yanastawi kona mbalimbali. Mazao haya yakilimwa kwa wingi kwa kufuata ushauri wa mafisa ugani tatizo la utapiamlo linaweza kumalizika kabisa.

UZALISHAJI WA MAZIWA

 Wakazi wa Wilaya ya Rungwe wanafuga mifugo mbalimbali. Ng’ombe wanafugwa takribani kila kaya. Afisa mifugo na Uvuvi wilaya ya Rungwe  Dr. Lawrance Kibona anabainisha kuwa wastani wa lita milioni 44 huzalishwa kila mwaka. Sawa na lita 140,000 kwa siku. Kila kaya hutumia lita mbili kama chakula na mengine huyauza kwa lengo la kukuza kipato cha kaya. Dr Kibona anafafanua kuwa kwa wastani kila kaya ina wakazi wanne hivyo kila mkazi hutumia nusu lita kwa siku na hivyo kujinasua na lindi la utapiamlo na udumavu kwa watoto hasa walio chini ya miaka miwili.

HALI YA LISHE KATIKA MKOA WA MBEYA

Hata hivyo akitoa takwimu za hali ya Lishe katika mkoa wa Mbeya katika kikao cha Afua za Lishe kilichofanyika mwezi desemba mwaka jana,  Afisa lishe mkoa wa Mbeya  bwana Benson  Sanga alisema kuwa kwa sasa udumavu kimkoa umepungua ambapo mwaka 1991 ulikadiriwa kufikia  asilimia 50 na mwaka 2018 umepungua kufikia asilimia 32 hali inayotia moyo na kupunguza tishio la kupata watoto wenye uwezo  mdogo wa kufikiri, kukosa umakini na  zaidi akina mama kupata shida wakati ya kujifungua na kupata watoto wenye ulemavu akitolea mfano ugonjwa wa mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE SEMINA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR December 19, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA AKIBA NAFASI YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI December 19, 2024
  • TANGAZO BARAZA LA MADIWANI April 27, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MKATABA June 10, 2021
  • Onesha Vyote

Habari Mpya

  • FURSA YA UTALII RUNGWE

    June 07, 2025
  • ELIMU YA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI YAHAMIA KIWIRA

    May 31, 2025
  • UTEKELEZAJI WA ILANI WAWASILISHWA

    May 30, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MIRADI

    May 30, 2025
  • Onesha Vyote

Video

Vivutio vya Utalii
Picha Mjongeo Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • TAMISEMI

Vinganishi Linganifu

  • OR TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Ufundi
  • Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma

Kipimo cha Wateja Duniani

world map hits counter

Wateja Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB

    Sanduku la Posta: Box 148

    Simu: 025 255 2586

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Huruhusiwi
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa