Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imefanya vizuri katika zoezi la chanjo ya polio ambapo zoezi hili limefanyika katika takribani mikoa Mitano ya Tanzania bara
Mikoa iliyoshiriki zoezi la chanjo ni pamoja na Mbeya, Katavi, Rukwa, Songwe, Kigoma na Kagera
Rungwe imechanja kwa asilimia 132.40% huku ikiwafikia watoto walio chini ya umri wa miaka 8 wapatao 114,832 na awali malengo yalikuwa kuchanja watoto 86,732 na hivyo chanjo imevuka malengo kwa asilimia 32.
Rungwe imeshika nafasi ya Pili baada ya Halmashauri ya Chunya huku ikifuatiwa na Mbeya jiji.
Katika zoezi hili Mkoa wa Mbeya umechanja jumla ya watoto 766,850 sawa na aslimia 124.82%
Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri kati ya Wananchi, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Watalamu wa afya, Vyombo vya habari na Wadau mbalimbali
Ugonjwa wa POLIO ambao kwa mara ya Mwisho Tanzania ilipata Mgonjwa wake mwaka 1996 hivi karibuni katika hatua nyingine Mgonjwa amegundulika Sumbawanga Mkoani Rukwa.
POLIO NINI?
POLIO ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya polio (poliovirus)
Ugonjwa huu humsababishia Mgonjwa kupooza viungo vya mwili na hatimaye kifo
Virusi vinaweza kuingia kwa njia ya mdomo kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na virusi hivyo
POLIO haina tiba lakini inaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya polio ya matone au sindano (IPV).
Ikumbukwe kuwa chanjo ya Polio haina madhara yoyote. Mtoto anaweza kupata chanjo ya polio mara nne au zaidi ili kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa huu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa