MAJUKUMU YA KITENGO CHA UHASIBU WA FEDHA
Mchango wa Halmashauri katika kugharamia utoaji huduma za kiuchumi na kijamii na mwelekeo wa kujitegemea bado uko chini sana. Mapato ya Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 ni kama inavyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo hapa chini:-
Jedwali Na. 9: Mapato Halisi ya Halmashauri (Tshs)
NA |
CHANZO CHA MAPATO |
MAKISIO 2015/2016 |
MAPATO HALISI JULAI– JUNI, 2016 |
% |
1 |
Mapato ya ndani
|
2,504,414,572.10 |
1,299,297,806.71 |
52 |
2 |
Matumizi Mengineyo
|
2,678,199,900.00 |
1,324,073,408.39 |
49 |
3 |
Mishahara
|
36,082,249,000.00 |
35,261,880,735.00 |
98 |
4 |
Miradi ya Maendeleo
|
9,895,193,174.31 |
4,895,014,343.68 |
49 |
5 |
Michango ya wananchi
|
450,000,000.00 |
484,577,827.58 |
108 |
|
Jumla Kuu
|
51,610,056,646.41 |
43,264,844,121.36 |
84 |
Chanzo: Idara ya Fedha ya Halmashauri, 2016
Kubuni vianzia vipya vya mapato katika Halmashauri sanjari na mchakato wa kupata sheria ndogo.
Kwa sasa vianzia vipya vilivyokwishabuniwa ni pamoja na:-
Ushuru wa Maziwa
Ushuru wa Samaki
Ushuru na Ada katika vyanzo vya Utalii
Ushuru wa Minara ya simu n.k.
Ada ya taka ngumu
Kupitia upya sheria ndogo za ukusanyaji mapato sanjali na ubadilishaji viwango Sheria zinazotumika sasa ni za mwaka 2012 , viwango vya ushuru vipo chini.
Kuwaendeleza watumishi wa Idara ya fedha.
Kufanya tathmini ya vyanzo vyote vya mapato ili kujua kiwango halisi kinachoweza kukusanywa na mbinu sahihi za kuweza kukusanya ushuru.
Kutoa elimu kwa walipa kodi, ushuru na ada mbalimbali juu ya umuhimu wa ulipaji ushuru huo kwa hiari.
Kushirikiana na wadau mbalimbali na taasisi za Serikali kama mahakama, polisi na TRA katika kufanikisha kukusanya mapato.
Kuhamasisha wakulima wa mazao mbalimbali kwa kutumia Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika waongeze uzalishaji wa mazao yaliyo bora na kuwatafutia masoko ya ndani na nje ya Wilaya.
Kupitia upya mikataba mbalimbali hususani ya upangishaji nyumba za Halmashauri na vibanda vya biashara ili iwe yenye kuiletea Halmashauri mapato zaidi na kuboresha nyumba hizo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa