Saturday 20th, April 2024
@Tukuyu
Mkuu wa Mbeya afanya Ziara Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe,alianza kwa kuongea na Watumishi wote wa Umma waliopo makao makuu ya Wilaya ya Rungwe, mkuatano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Leo tarehe 13/09/2018.
Aidha baada ya Mkutano huo alielekea Chuo cha Ualimu Mpuguso kutembelaea ujenzi wa wa mabweni, madarasa na nyumbani za watumishi ambapo ujenzi huo umegharimu kiasi cha tsh.bilioni 9.6.
Baada ya kutembelea ujenzi katika Chuo hicho alielekea katika Uwanja wa Mpira Tandale uliopo Tukuyu Mjini kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Wilaya ya Rungwe.
Katika mkutano huo Mkuu Wa Wilaya ya Rungwe Mh.Julius Chalya alitoa taarifa mbalimbali za maendeleo katika Wilaya ya Rungwe katika Sekta za Afya,Elimu,Barbara,Maji,Kilimo,Mifugo na suala zima la ukusanyaji mapato.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa