Friday 19th, April 2024
@Ukumbi wa Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.Loema I.Peter aligawa Vitabu vya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2015 kwa Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Lengo la kugawa vitabu hivyo vya utekelezaji wa Ilani ni kuwakumbusha wajibu wao na kutekeleza kwa kufuata ilani hizo.
Ilani hizo alizigawa kwa Wakuu hao ambao ndiyo wasisimamizi katika Idara na Vitengo ili ziweze kuwambusha na kufuata Ilani hiyo katika kutekeleza wajibu na majukumu yao katika kazi; Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza kwa kusema "ilani hizi nawapa zikawasaidie katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku na wale ambao wamesahau au wanazembea basi zikawakumbushe wajibu wao, pia mkawasimamie na watumishi wote walio katika Idara na Vitengo vyenu kwa kuwakumbusha kufanya kazi kwa weredi na juhudi katika kutekeleza ilani ya chama". Vitabu hivyo vya Ilani aligawa tarehe 31/12/2018 alipokuwa katika kikao cha kawaida na wakuu wa Idara na vitengo ambacho hufanyika kila juma tatu asubuhi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Aidha kupitia kikao hicho aliwataka wakuu wa idara na Vitengo kwa kushirikiana na watumishi ambao wapo katika idara/vitengo vyao wafanye tathmini ya utendaji wao wa kazi kwa mwaka 2018 kwa kurejea malengo waliyojiwekea wakati mwaka unaanza kufanya marekebisho pale walipo feli na kuongeza juhudi zaidi pale walipo faulu na pia waweke malengo mengine kwaajili ya mwaka 2019. Wakuu wa Idara/Vitengo walishukuru sana kupewa ilani hizo na kuahidi kuongeza juhudi kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Picha: Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakipokea Vitabu vya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2015. kutoka kwa Mkurugenzi wa Halamshauri ,Ilani hiyo ndiyo inayotekelezwa sasa na Serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.
(picha zote na Suzan Mhoja)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.loema I.Peter akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa