Wednesday 24th, April 2024
@Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Julius Chalya anawatangazia na kuwakaribisha wananchi wote kuwa tarehe 18/5/2019 Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika kata ya Kisiba ukitokea Halmshauri ya Busokelo. Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi 8 kwa kuweka mawe ya msingi, uzinduzi ,kukagua na kutembelea. Miradi hiyo ipo katika kata za Kisiba, Ilima, Bagamoyo,Lufingo ,Iponjola na Kyimo. Baada ya kumaliza shughuli hizo za kuweka mawe ya msingi,uzinduzi,ukaguzi na kutembelea. Pia utatoa mikopo kwa vikundi 11 vya wanawake,vijana na walemavu. Mwenge wa Uhuru Utakesha katika kata ya Kiwira. Wananchi wote mnaombwa kujitokeza kushiriki katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru ambao, utaondoka Wilaya ya Rungwe tarehe 19/05/2018 na kukabidhiwa Wilaya ya Mbeya Vijijini katika kijiji cha Maganjo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa