Wednesday 24th, April 2024
@Tukuyu youth center
TAMASHA ni taasisi isiyo ya kiserikali inayo endesha mradi wa Feed the future (inua vijana), katika mradi huo wanatoa mafunzo ya afya, ujinsia na stadi za maisha kwa vijana ambao wapo katika makundi ambayo ni wawakilishi wa makundi hayo katika Kata na vijiji. Mafunzo hayo yanatolewa kwa njia ya mbinu shirikishi (participatory theory).
Mafunzo yalianza tarehe 23/04/2019 katika ukumbi wa Tukuyu Youth Center uliopo Tukuyu Mjini. Lengo la mafunzo hayo ni vijana viongozi waliopata mafunzo hayo kwenda kufundisha makundi hayo katika sehemu walizotoka. Jumla ya washiriki 57 walipata mafunzo hayo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa